Kuswali faradhi ndani ya Ka´bah

Swali: Kuswali faradhi ndani ya Ka´bah.

Jibu: Kuna makinzano. Maoni ya sawa ni kwamba hakuna neno kuswali ndani yake. Swalah ni sahihi ingawa baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali ndani yake. Msingi ni kwamba ikifaa kuswali swalah inayopendeza itafaa pia kuswali faradhi. Huu ndio msingi isipokuwa kukiwepo dalili. Lakini Sunnah na kilichowekwa katika Shari´ah ni kwamba imamu na watu wanaswali faradhi nje ya Ka´bah, kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23593/هل-تجوز-صلاة-الفريضة-داخل-الكعبة
  • Imechapishwa: 16/02/2024