Inafaa kwa Mtume pekee kuelekea Qiblah wakati wa kukidhi haja?

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa kumuona kwake Ibn ´Umar Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikidhi haja kuelekea Qiblah ni jambo maalum kwake na hivyo hakuna hoja juu yake.

Jibu: Hapana, maneno haya hayana mategemezi. Kitendo chake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni dalili. Maneno yake pia ni dalili:

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا

“Hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho na akamtaja Allaah kwa wingi.”[1]

Swali: Vipi wakati maneno yanapingana na kitendo?

Jibu: Maneno ndio yanayotangulizwa mbele. Lakini kitendo kinafasiri maneno; ya kwamba sio lazima. Mtu akiwa sehemu ya wazi ni wajibu [kukiepuka]. Akiwa ndani ya nyumba sio lazima [kukiepuka]. Hata hivyo akiacha kuelekea Qiblah ndani ya nyumba inakuwa ni vyema zaidi – Allaah akitaka. Kama alivosema Abu Ayyuub:

“Tunakiepuka na kumuomba Allaah msamaha.”

[1] 33:21

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23579/هل-يجوز-استدبار-الكعبة-في-قضاء-الحاجة
  • Imechapishwa: 16/02/2024