Kuswali Dhuhr baada ya kumaliza kuswali ijumaa

Baadhi ya watu hivi katika zama zilizokuja nyuma ikiwa katika mji mmoja kuna mikusanyiko miwili na zaidi basi wanaswali Dhuhr baada ya swalah ya ijumaa na wanadai kwamba kufanya hivo kuna kuchukua tahadhari kwa kuchelea kutosihi moja kati ya ijumaa mbili hizo. Ukweli wa mambo ni kwamba haya ni maovu ya wazi na uzushi katika Uislamu ambao kuukubali. Wamelikemea waliokutana nalo katika wale wanazuoni wakaguzi. Kwa sababu Allaah (Subhaanah) amewawajibishia waislamu katika siku ya ijumaa na nyenginezo swalah tano ilihali watu wanawawajibishia watu siku ya ijumaa kuswali swalah sita. Haijalishi kitu hata kama hawatowajibisha jambo hilo bali wamelipendekeza au kuliruhusu. Yote hayo hayajuzu. Kwa sababu ni miongoni mwa Bid´ah zilizozuliwa. Imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa akisema katika Khutbah ya ijumaa:

“Mazungumzo bora ni Kitabu cha Allaah, uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa na kila Bid´ah ni upotofu.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”[2]

Muslim ameipokea kwa tamko lisemalo:

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[3]

[1] Muslim (1435) na Ibn Maajah (44).

[2] al-Bukhaariy (2499) na Muslim (3242).

[3] Muslim (3243).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/90)
  • Imechapishwa: 22/10/2021