Kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah katika Rak´ah ya tatu na ya nne

Swali: Vipi kuhusu kusoma kwenye Rak´ah ya tatu na ya nne katika swala ya ´ishaa baada ya al-Faatihah?

Jibu: Ni kama katika Dhuhr na ´Aswr. Hatufahamu dalili yoyote inayosema kinyume na hilo. Ni kama kusoma al-Faatihah tu katika Dhuhr na ´Aswr.

Swali: Nini kinachosomwa katika ´Aswr kwenye Rak´ah ya tatu na ya nne?

Jibu: Udhahiri wa Sunnah ni kwamba kunasomwa al-Faatihah peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24841/ما-حكم-القراءة-في-الاخيرتين-بالصلاة-الرباعية
  • Imechapishwa: 20/12/2024