Kusoma Qur-aan ndani ya nyumba kabla ya kuhamia ndani yake

Swali: Baadhi ya watu wanapojenga nyumba kabla ya kuhamia huleta wasomaji wa Qur-aan wasome ndani yake. Je, hili lina msingi?

Jibu: Sifahamu kuwa lina msingi wowote. Sifahamu kitu chochote kuhusu hilo. Lakini kusoma Qur-aan kuna manufaa, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika shautwaan hukimbia nyumba inayosomwa Suurah al-Baqarah.”

“Fanyeni baadhi ya swalah zenu ndani ya majumba yenu, kwani zinaimarishwa kwa kisomo, utajo wa Allaah na swalah.”

Hili ni jambo linalotakikana.

Swali: Vipi ikiwa mtu atafanya hivyo kama desturi kila anapojenga nyumba au wakati fulani?

Jibu: Sifahamu kuwa lina msingi.

Swali: Je, inaweza kusemwa kuwa ni Bid´ah?

Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Pengine ni bora zaidi kuachana nalo. Akifanya hivo bwana mwenye nyumba… Kuhukumu jambo hilo kama Bid´ah kunahitaji mazingatio ya kina.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24823/حكم-قراءة-القران-في-البيت-قبل-السكن-فيه
  • Imechapishwa: 22/12/2024