Kusoma kwa mtu asiyemfanyia Tabdiy´ ´Ar´uur, al-Ma´ribiy na al-Maghraawiy

Swali: Inajuzu kuchukua elimu kwa mtu ambaye hambadiy´ ´Ar´uur, Abul-Hasan al-Ma´ribiy na al-Maghraawiy na anasema taasisi ya Ihyaa’ at-Turaath ni Salafiy?

Hajasoma na wala hana Tazkiyyah kutoka kwa wanachuoni. Anachukua elimu kwenye kanda na vitabu vya Ibn Baaz, al-Albaaniy na Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahumu Allaah).

Jibu: Kwa hakika ni kwamba yule ambaye hawafanyii Tabdiy´ watu hawa, yeye ni kama wao. Kwa kuwa watu hawa ni watu wa Bid´ah. Na al-Maghraawiy imethibiti kwake kuwa ni Takfiyriy.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=865
  • Imechapishwa: 20/07/2020