Swali: Wafuasi wa al-Maghraawiy wanatumia kama hoja mapendekezo ya Shaykh Saliym al-Hilaaliy na Shaykh ´Aliy al-Halabiy, kwa kuwa watu wote hawa wawili wanamtetea al-Maghraawiy na Ma´ribiy. Je, watu hawa wanaingia katika wao au tufanye nini?

Jibu: Yule mwenye kuwatetea wazushi anaingia katika wao. al-Maghraawiy kumethibiti uthibitisho usiokuwa na shaka ndani yake.

Kuhusu al-Maghraawiy, imetuthibitikia pasi na shaka yoyote kuwa anasema kwamba Uislamu wa pamoja umekatika tangu hapo kitambo na kwamba hii leo kuna Uislamu wa mtu mmojammoja. Hivo ndivo anavosema. Vivyo hivyo anasema kuwa yule mwenye kumtii mke wake katika jambo la haramu, basi amemfanya kuwa ni mungu. Hii maana yake ameritadi na kutoka nje ya Uislamu. Tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alnajmi.net/voices.php?action=show&id=54
  • Imechapishwa: 20/07/2020