Kusoma katika Rak´ah ya tatu na ya nne baada ya al-Faatihah

Swali: Vipi kusoma Suurah fupi katika Rak´ah ya tatu na Rak´ah ya nne baada ya al-Faatihah?

Jibu: Asome al-Faatihah peke yake. Isipokuwa Dhuhr peke yake ni sawa akisoma baadhi ya nyakati nyongeza katika Rak´ah ya tatu na Rak´ah ya nne, kwani kumepokelewa katika Hadiyth ya Abu Sa´iyd yanayofahamisha juu ya hilo.

Swali: Haikuthibiti kwa Abu Bakr as-Swiddiyq inapokuja katika Maghrib?

Jibu: Imepokelewa kutoka kwa as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alisoma katika Rak´ah ya tatu:

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا

“Ee Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza.”[1]

[1] 03:08

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23742/حكم-القراءة-بعد-الفاتحة-في-الثالثة-والرابعة
  • Imechapishwa: 18/04/2024