Kusoma Aayah kwa idadi maalum ili mtu apate alichokipoteza

Swali: Mtu akipoteza kitu na akasema:

إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ

“Hakika Yeye juu ya kumrudisha kwake bila shaka ni muweza.” (86:08)

mara mia moja. Je, kitamrudilia alichokipoteza au hapana?

Jibu: Hilo halikuthibiti katika Qur-aan na Sunnah. Vilevile sio katika sababu za kawaida zenye kufanya kilichopotea kikarudi. Ni katika kuitumia Qur-aan kwenye mambo ambayo hayakuteremshwa kwa ajili yake. Isitoshe pamoja na kuweka kiwango cha idadi maalum. Kuweka idadi ya kiwango maalum ni jambo linalokuwa kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah peke yake na si jambo linalojulikana kwa kutumia akili. Hivyo kufanya hivo ni Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuzua katika dini yetu hii yasiyokuwemo, atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/69)
  • Imechapishwa: 23/08/2020