Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 06

57 – al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Ahmad bin Mansuur ametuhadithia: Shurayh bin an-Nu´maan ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr aliyesema:

“Namshuhudilia Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy kwamba wawili hao wamemshuhudilia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema: “Allaah (´Azza wa Jall) anatoa muhula mpaka kunapopita theluthi ya usiku ndipo hushuka na husema: “Je, kuna mwenye kuomba apewe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha kutokamana na dhambi? Je, kuna mwenye kuomba ajibiwe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 134
  • Imechapishwa: 26/04/2020