48 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: Ya´quub bin Ishaaq al-Faluusiy ametuhadithia: Bakr bin Yahyaa bin Zibaan ametuhadithia: Musaddad ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Ishaaq, kutoka kwa Sa´iyd al-Maqbariy, kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapopita nusu ya usiku ya kwanza basi Allaah (´Azza wa Jall) anashuka katika mbingu ya dunia na anasema mpaka alfajiri inaingiai: “Hakuna mwenye kuuliza apewe? Hakuna mwenye kuomba ajibiwe? Hakuna mgonjwa aponywe? Hakuna mtenda dhambi mwenye kuomba msamaha asamehewe?”

Muhammad bin Abiy Bakr bin ´Adiy pia ameipokea kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq Sa´iyd al-Maqbariy ambaye amesema: Kutoka kwa ´Atwaa’, mtumwa wa Umm Swafiyyah, kutoka kwa Abu Hurayrah. Kumejitokeza kosa la chapa hapo. Sahihi ni mtumwa wa Umm Swubayyah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 128
  • Imechapishwa: 09/03/2020