23- Abu Muhammad bin Sa´iyd alisomewa na huku mimi nasikiliza: ´Abdullaah bin ´Amr al-´Aabidiy al-Makhzuumiy amekuhadithieni Makkah: Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia…

´Ubaydullaah bin Sa´d az-Zuhriy pia ametuhadithia: Ami yangu ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu ´Abdillaah al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyeeleza kuwa alimweleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kila usiku katika mbingu ya dunia wakati kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie? Ni nani aniulizaye nimpe?”

Kwa ajili hiyo ndio maana kumependekezwa kuswali sehemu ya mwisho ya usiku kuliko ya mwanzo.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 18/12/2019