Kusema tu لا حول bila kuikamilisha

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema:

لا حول

”Hakuna uwezo.. ”

bila kukamilisha kwa kusema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni kusema kikamilifu:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”

Haifai kuishia kwenye:

لا حول

”Hakuna namna… ”

Bali aiseme kikamilifu. Huo ndio mwendo wa Sunnah:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”

Akisema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”

na hakuweza kusema yote kwa kukusudia kuonyesha udhaifu wake mwenyewe, hapana kosa. Lakini Sunnah ni kuileta kamili:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”

Swali: Baadhi ya watu husema:

لا حول الله

”Hakuna uwezo wa Allaah.”?

Jibu: Afundishwe, ni mtu wa kawaida, afundishwe maneno sahihi.

Swali: Anakusudia kwamba baadhi ya watu wa kawaida husema:

لا حول الله

”Hakuna uwezo Allaah.”?

Jibu: Afundishwe kusema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”

Maana yake ni sina uwezo wa kubadilisha chochote isipokuwa kwa msaada wa Allaah, au sina nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Lakini akishafahamu huambiwa aikamilishe kwa kusema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

”Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah.”

Afundishwe mwendo wa Sunnah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31686/ما-حكم-من-يقول-لا-حول-ولا-يكمل-الحوقلة
  • Imechapishwa: 05/12/2025