Kusema ”Lirabbiyya al-Hamd” wakati wa kuinuka kwenye Rukuu´

Swali: Vipi ikiwa mtu atasema:

لربي الحمد، لربي الحمد

”Himdi ni kwa Mola wangu, himdi ni kwa Mola wangu.”

bila kusema sifa nyingine nne zilizotajwa?

Jibu: Hapana vibaya juu yake. Hata hivyo kilicho bora ni kusema kile kilichoelezwa katika Hadiyth Swahiyh, kama kusema:

ربنا ولك الحمد

“Mola wetu, na himdi zote njema ni Zako.”[1]

na:

اللهم ربنا ولك الحمد

“Ee Allaah, Mola wetu, na himdi zote njema ni Zako.”[2]

Ni vyema mtu kuzingatia na kufuata yaliyotajwa katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh.

[1] al-Bukhaariy (689) na Muslim (392).

[2] al-Bukhaariy (796).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24848/حكم-قول-لربي-الحمد-عند-الرفع-من-الركوع
  • Imechapishwa: 02/01/2025