Kuongeza “wa Barakaatuh” katika salamu ya swalah II

Swali: Nini hukumu ya kuongeza maneno:

وبركاته

“… na baraka Zake.”

katika salamu ya kumaliza swalah?

Jibu: Dhaifu, yanapingana na yaliyo Swahiyh. Masimulizi hayo yanahitaji kuangaliwa vyema. Yana udhaifu. Kilicho Swahiyh na kilichohifadhiwa ni kuishilia kusema:

ورحمة الله

”… na rehema za Allaah.”

kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn Mas’uud, Samurah bin Jundub na Sa’ad bin Abiy Waqqaas. Ingawa al-Haakim (Rahimahu Allaah) ameisahihisha, lakini bado kuna shaka juu ya usahihi wake kwa sababu inatokana na masimulizi ya ´Alqamah kwa kunukuu kwa njia isiyokuwa wazi na hakusikia moja kwa moja kutoka kwa baba yake. Kwa ajili hiyo Ibn Ma’iyn na wanazuoni wengine wamesema kuwa ´Alqamah hakuisikia kutoka kwa baba yake, ingawa baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa amesikia baadhi ya mambo kutoka kwake. Hata hivyo baadhi ya masimulizi ndani ya ”as-Swahiyh” ya Muslim zinataja kwamba ´Alqamah alisikia kutoka kwa baba yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24863/حكم-زيادة-وبركاته-في-التسليم-من-الصلاة
  • Imechapishwa: 02/01/2025