Hekima ya kukatazwa kuingia vidole vya kulia ndani ya vidole vya kushoto

Swali: Kuna hekima gani ya kukatazwa kuingiza vidole vya kulia ndani ya vidole vya kushoto?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. ash-Shawkaniy ametaja kwamba imesemekana ni aina ya upuuzi. Wengine wakasema kwamba ni kitendo cha shaytwaan, lakini maoni hayo yanahitaji dalili.

Swali: Je, sababu ni kwamba mtu huyo yuko ndani ya swalah?

Jibu: Anapokuwa anatoka kwenda kuswali, anachukuliwa kama yuko ndani ya swalah… Ni jambo lisiloendana na swalah. Si jambo la ajabu kwamba hekima ya hili haipaswi kujulikana kila wakati, lakini mtu analazimika kutii hata kama hajui hekima yake.

Swali: Lakini si kuna masimulizi yanayosema:

“Yuko  ndani ya swalah.”?

Jibu: Ndiyo, inamaanisha kuwa  pale anapokuwa anatoka. Kwa hivyo ikafahamisha kuwa asifanye hivo ndani ya swalah. Kuhusu hekima ya kukatazwa ni kwa sababu ya upuuzi au ni kitendo cha sahytwaan? Hakuna ishara ya upuuzi wa moja kwa moja, kama ilivyosemwa. Lakini Shari´ah inajua zaidi na ni yenye hekima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24866/الحكمة-من-النهي-عن-تشبيك-الاصابع-عند-الخروج-الى-الصلاة
  • Imechapishwa: 02/01/2025