Imamu anaendelea kuswali licha ya kwamba amekumbuka nguo yake inayo najisi

Swali: Vipi ikiwa mtu ni imamu ambaye amejua kuwa kuna najisi katika suruwali yake kisha akaendelea kuswali?

Jibu: Imamu anapaswa kurudia swalah yake, lakini maamuma hawapaswi kurudia swalah yao.  Kwa sababu wao hawakujua kuhusu najisi hiyo. Hata hivyo ilimlazimu imamu kuteua mbadala wake [pale alipojua kuwa anayo najisi].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24909/حكم-الصلاة-اذا-علم-الامام-ان-في-ثوبه-نجاسة
  • Imechapishwa: 02/01/2025