Kusalimia kwa kuashiria tu

Swali: Vipi kusalimia kwa kuashiria?

Jibu: Kwa kutamka. Lakini ikiwa mtu yuko kwa mbali basi amwashirie ili mtu ajue kuwa anasalimiwa. Aliwapitia wanawake akawaashiria. Muhimu ni kwamba akihitajia kuashiria kutokana na umbali wao, uchache wa kusikia kwao, basi awaashirie sambamba na kuzungumza. Vinginevyo haijuzu kusalimia kwa kuashiria tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23939/هل-يجوز-السلام-بالاشارة-دون-كلام
  • Imechapishwa: 02/08/2024