Kupita mbele ya mswaliji katika msikiti wa Makkah


Swali: Ni ipi hukumu ya kupita mbele ya mswaliji katika msikiti Mtukufu wa Makkah? Je, ni sawa kwa mswaliji kumzuia anayepita mbele yake?

Jibu: Hapana neno katika hilo. Si sawa kwa ambaye yuko katika msikiti Mtakatifu wa Makkah kumzuia anayetaka kupita mbele yake kutokana na zile Aathaar zilizopokelewa zinazojulisha kwamba Salaf hawakuwa wakiwazuia wanaopita mbele yao katika msikiti Mtakatifu ambao ni wale wenye kutufu na wengineo. Miongoni mwao ni Ibn-uz-Zubayr (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Isitoshe msikiti Mtakatifu wa Makkah ni mahali kumejaa msongamano na haiwezekani kumzuia anayepita mbele ya mwenye kuswali. Kwa hivyo ikawalazimika kufanya wepesi katika hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/102)
  • Imechapishwa: 14/10/2021