Swali: Mwanamke huyu amefanyiwa chuku na ambaye amemfanyia amemwambia kuwa amepatwa na kijicho na kwamba chuku ni sababu ya kupona…

Jibu: Huu ni uongo. Kuumikwa sio tiba ya kijicho. Kufanya chuku ni dawa ya maradhi. Ni kweli kwamba ni tiba na ni miongoni mwa tiba za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini kusema kuwa ni tiba ya kijicho ni uongo. Huyu anachotaka ni kuwavuta watu na wakusanyike kwake ili achukue pesa zao. Haya ndio malengo yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 21/04/2021