Swali: Ambaye anapika nyama yake ya Udhhiyah na akawapa ndugu na majirani zake hali ya kuwa tayari imeshapikwa anazingatiwa ametekeleza Sunnah?

Jibu: Kilichopendekezwa katika ´Iyd-ul-Adhwhaa ni yeye na familia yake wale na kuhifadhi sehemu yake, wawape swadaqah mafukara na masikini na wawazawadie jamaa na majirani. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ

“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu nyama za Udhhiyah:

“Kuleni, hifadhini na toeni swadaqah.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh

Bakr Abu Zayd

[1] 22:28

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18002)
  • Imechapishwa: 27/07/2020