Swali: Je, inajuzu kupeana mikono na mayahudi na manaswara?

Jibu: Sijui kama kuna ubaya wowote wa kufanya hivo. Akikupa mkono na wewe mpe mkono kama jinsi akianza kukusalimia na wewe msalimie. Na Allaah ndiye Anajua zaidi.

Kuna mambo tuliyopitia na hatukuyajibu. Je, wao wakitupa hongera kwa sikukuu zetu na sisi tuwape hongera kwa sikukuu zao? Jibu ni hapana. Haijuzu kwetu kuwapa hongera kwa sikukuu zao. Kwa sababu huku ni kukubaliana na wao katika sikukuu zao za kikafiri. Haijuzu kwa Muislamu kuwapa hongera makafiri kwa sikukuu zao, kuwasaidia, kuwapa sehemu wakafanya sikukuu wala kuwachanga kwa pesa wakafanya sikukuu zao. Asiwasaidii na wala asiwape hongera kwa sikukuu zao. Kwa kuwa ni sikukuu za kikafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-7-20.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015