Du´aa ya kafiri aliodhulumiwa inapokelewa?

Swali: Du´aa ya kafiri ni yenye kuitikiwa ikiwa amedhulumiwa?

Jibu: Ndio. Du´aa ya mwenye kudhulumiwa ni yenye kupokelewa hata kama ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Iogope du´aa ya mwenye kudhulumiwa. Kwani hakika hakuna baina yake na baina ya Allaah kizuizi.”

Hili linamuhusu muislamu na kafiri wote wawili. Allaah Anamuitikia du´aa kafiri wakati fulani kama katika hali anapokumbwa na dhiki. Hali kadhalika Allaah Anamuitikia du´aa yake wakati ambapo ni mwenye kudhulumiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-7-20.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015