Swali: Tumegundua kwa wahudhuriaji kwamba kila wanaposikia kutoka kwa Shaykh akisema: “Laa ilaaha illa Allaah”, wao pia husema: “Laa ilaaha illa Allaah” kwa kupaza sauti kiasi fulani. Je, haitoshi kuamini moyoni bila kuinua sauti mara kwa mara kila linapotajwa tamko la “Laa ilaaha illa Allaah”? Je, jambo hili ni Bid´ah au si Bid´ah?
Jibu: Ama yale wanayofanya Suufiyyah kwa kupaza sauti ya pamoja, wakikusanyika na kuinua Dhikr kwa sauti za pamoja, hilo ni katika Bid´ah. Ama mtu kumtaja Allaah na mwingine kumtaja Allaah, na anaposikia anayemtaja Allaah naye akamtaja Allaah kwa sababu amekumbushwa na ndugu yake, basi hilo hakuna ubaya ndani yake. Hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wametangulia al-Mufarriduun.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah, ni nani hao al-Mufarriduun?” Akasema: “Ni wale wanaume na wanawake wanaomtaja Allaah kwa wingi.”
Kumtaja Allaah kunatakiwa daima. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ
”Anayejifanya kipofu na ukumbusho wa Mwingi wa rehema, basi Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake mwandani.”[1]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
“Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru na msabihini asubuhi na jioni.”[2]
Kwa hiyo inampasa muumini azidishe kumtaja Allaah kila mahali. Anaposikia Dhikr kutoka kwa ndugu zake huamka na kumtaja Allaah kama walivyomtaja ndugu zake. Hili ni jambo linalotakiwa. Vivyo hivyo kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumsalimia, inatakiwa kuzidisha hilo.
Lakini jambo la kupanga utaratibu maalum kwa sauti ya pamoja, hilo ndilo linalokanushwa, nalo ni Bid´ah. Hilo ndilo wanalolifanya Suufiyyah. Jambo kama hilo lilifanywa zamani na kundi fulani katika zama za Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) katika zama za Maswahabah ambapo Ibn Mas´uwd (Radhiya Allaahu ´anh) akawakemea.
[1] 43:36
[2] 33:41-42
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3401/حكم-رفع-الصوت-جماعيا-بالذكر-من-غير-تواطو
- Imechapishwa: 13/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3401/حكم-رفع-الصوت-جماعيا-بالذكر-من-غير-تواطو
Imechapishwa: 13/09/2026
https://firqatunnajia.com/kupandisha-sauti-juu-wakati-wa-kumtaja-allaah/