Swali: Ikiwa jukumu la msingi la kila muislamu ni kulingania kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa kufuata mfano wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake, basi ni nasaha gani mnazowapa wanazuoni kuhusu kuunga mkono na kusaidia kundi linalojitolea, kwa kuwa katika hali ya kulegalega kwetu katika ulinganizi huu, hilo litakuwa kwa faida ya shughuli za wamisionari na walinganiaji wa batili na kuwa sababu ya ghadhabu ya Allaah na kushuka kwa adhabu na misiba?
Jibu: Imeshatangulia katika sehemu hii mara nyingi kwamba wajibu juu ya wanazuoni ni kushirikiana katika jambo hili, kwamba wajibu juu ya kila mwanazuoni na kila mwenye elimu ni kulingania kwa Allaah (´Azza wa Jall), kueneza dini na kuvumilia katika hilo, hata bila ya ujira, hata bila ya malipo. Malipo yako kwa Allaah (´Azza wa Jall). Walikuwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wakilingania Allaah bila ya malipo. Vivyo hivyo Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) walikuwa wakilingania Allaah bila ya malipo:
وقُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا
“Sema: ”Sikuombeni malipo kwa hayo.”[1]
قُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ
”Sema: ”Malipo yoyote kama nimekuombeni basi huo ni wenu. Sina malipo isipokuwa kwa Allaah tu.”[2]
Hivyo wanazuoni na watu wa kheri jukumu lao ni kulingania kwa Allaah katika kila mahali, kulingana na elimu waliyonayo, wanusuru haki na wawasaidie ndugu zao walinganiaji katika kila mahali ili haki ishinde, ili neno liungane, ili ajifunze asiyejua na ili aongoke aliyepotea. Ama kulegalega huku si katika dini. Bali ni miongoni mwa yale anayoyapamba shaytwaan na anayoyaita shaytwaan. Kwa hiyo haijuzu kulegalega katika kulingania kwa Allaah kwa watu wa elimu. Ni wajibu wao kulingania kwa Allaah katika kila mahali, ni mamoja wawe ni mahakimu au waalimu, au si mahakimu wala waalimu, lakini wana elimu, basi katika hali hiyo ni juu yao ni kutoa juhudi zao kadiri ya uwezo:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[3]
Katika nchi zao na nje ya nchi zao, pamoja na ndugu zao walinganiaji wanawahamasisha, wanawanusuru, wanashauriana nao na wanakumbushana nao katika kila jambo linaloweza kufichika ili ulinganizi uwe mmoja wenye kushikamana, wakishirikiana, wakisaidiana na wakielewana. Ikiwa mmoja wao atakosea, mwingine amuonye na aelewane naye ili uhasama uondoke, ili ipatikane ushirikiano na ili makosa yasahihishwe na yaondolewe. Hivyo ndivyo ulivyo wajibu juu ya wanazuoni.
[1] 06:90
[2] 34:47
[3] 64:16
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3406/وجوب-الدعوة-الى-الله
- Imechapishwa: 13/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3406/وجوب-الدعوة-الى-الله
Imechapishwa: 13/09/2026
https://firqatunnajia.com/uwajibu-wa-kila-muislamu-kulingania-kwa-allaah/