103 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz ametukhabarisha, kutoka kwa Sahl, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa juu ya Hiraa’ pamoja na Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah na az-Zubayr. Jabali likaanza kutikisika ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Tulia! Hakuna juu yako isipokuwa Mtume, mkweli au shahidi.”

104 – Muhammad bin al-´Alaa’ ametukhabarisha: Ibn Idriys ametukhabarisha: Huswayn ametukhabarisha, kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf, kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim… Na kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Hilaal, kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim (Sufyaan amemtaja bwana mmoja baina yake yeye na ´Abdullaah bin Dhwaalim): Nimemsikia Sa´iyd bin Zayd akisema:

“Wakati Mu’aawiyah alipofika Kuufah, Mughiyrah bin Shu’bah alisimama akitoa Khutbah ya kumtukana ´Aliy. Sa’iyd bin Zayd akanishika mkono wangu na kusema: “Huoni dhalimu huyu anayeamrisha kumlaani mtu ambaye ni katika watu wa Peponi? Ninashuhudia kwamba wale tisa wako Peponi na ningelitaka basi naweza pia kutoa ushahidi wa mtu wa kumi.” Nikasema: “Ni kina nani hao tisa?” Akasema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa juu ya Hiraa’ akasema: “Tulia! Hakuna juu yako isipokuwa Mtume, mkweli au shahidi.” Akasema: “Ni kina nani hao tisa?”  Akasema: “Mtume wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimaja Abu Bakr, Umar, `Uthmaan, `Aliy, Twalhah, az-Zubayr, Sa’d na `Abdur-Rahmaan.” Nikasema: ”Ni nani wa kumi?” Akasema: “Mimi.”[1]

[1] Muslim (2417).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 13/09/2026