100 – Qutaybah bin Sa´iyd amenikhabarisha: ´Abdul-Waahid ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hasan bin ´Ubayd: al-Hurr bin Swabbaah ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Akhnas: Sa´iyd bin Zayd alisimama na kusema: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, ´Uthmaan yuko Peponi, Twalhah yuko Peponi, az-Zubayr yuko Peponi, Sa´d yuko Peponi na ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf yuko Peponi.” Ningelitaja kumtaja wa tisa basi ningelimtaja.” Tukafikiri anajikusudia yeye mwenyewe.”

101 – Muhammad bin al-Muthannaa na Muhammad bin Bashshaar wametukhabarisha: Ibn Abiy ´Adiy ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Huswayn, kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf, kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim, ambaye ameeleza:

“al-Mughiyrah bin Shu´bah alitoa Khutbah na akamtukana ´Aliy, ambapo Sa´iyd bin Zayd akasema: “Nashuhudia ya kwamba nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Tulia, ee Hiraa’! Hakuna aliye juu yako isipokuwa Mtume, mkweli au shahidi.” Juu yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, Sa´d na ´Abdur-Rahmaan na Sa´iyd bin Zayd.”

Hilaal bin Yasaaf hakuyasikia haya kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim.

102 – Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Umar amenikhabarisha: Qaasim al-Jarmiy ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf, kutoka kwa Fulaan bin Hayyaan, kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim, ambaye amesimulia:

”Nilisimama mbele ya Sa´iyd bin Zayd, akasema: ”Viongozi wetu wanatuamrisha tuwalaani ndugu zetu, lakini sisi hatuwalaani, bali tunasema: “Allaah awasamehe.” Kwani nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Kutakuwako baada yangu fitina zitazokuwa na haya na yale.” Bwana mmoja akasema: “Tukikutana nazo, basi bila shaka tutaangamia.” Akasema: ”Itakutosheni mfe.” Kisha akaja bwana mmoja na kusema: ”Mimi nampenda ´Aliy na sikuwahi kumpenda hata kidogo.” Akasema: ”Unampenda mtu kutoka katika watu wa Peponi.” Kisha akaanza kuzungumza na kusema: ”Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, ´Abdur-Rahmaan, Sa´d na ningelitaka basi ningelimtaja wa tisa, ambapo akasema: ”Tulia, ee Hiraa´! Kwani hakuna juu yako isipokuwa Mtume, mkweli au shahidi.” Alikuwa anajikusudia yeye mwenyewe.”

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 80
  • Imechapishwa: 13/09/2026