99 – Muhammad bin Bashshaar ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan ametukhabarisha: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Abu Haashim, kutoka kwa Abu Mijliz, kutoka kwa Qays bin ´Abbaad, amabye amesema:

”Nimemsikia Abu Dharr akiapa juu ya Aayah isemayo:

هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ

”Hawa ni wapinzani wawili wanabishana juu ya Mola wao.”[1]

kwamba imeteremshwa kuhusu ´Aliy, Hamzah, ´Ubaydah bin al-Haarith, Shaybah bin Rabiy´ah na ´Utbah bin Rabiy´ah. Walizozana siku ya Badr.”[2]

[1] 22:19

[2] al-Bukhaariy (3969).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 79
  • Imechapishwa: 13/09/2026