91 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Humayd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, ´Uthmaan yuko Peponi, ´Aliy yuko Peponi… ”
Imekuja katika upokezi mwingine:
“Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, ´Aliy yuko Peponi, ´Uthmaan yuko Peponi, Twalhah yuko Peponi, az-Zubayr yuko Peponi, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf yuko Peponi, Sa´d bin Abiy Waqqâs yuko Peponi na Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah yuko Peponi.”
92 – Muhammad bin Abaan ametukhabarisha: Muhammad bin Ismaa´iyl bin Abiy Fudayk ametukhabarisha, kutoka kwa Muusa bin Ya´quub bin ´Abdillaah bin Wahb bin Zam´ah, kutoka kwa ´Umar bin Sa´iyd, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Humayd, kutoka kwa baba yake, aliyesimulia kwamba Sa´iyd bin Zayd alimweleza mbele ya umati kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Kumi wako Peponi: Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, ´Abdur-Rahmaan, Abu ´Ubaydah bin ´Abdillaah na Sa´d bin Abiy Waqqaas.” Akawahesabu hawa kumi kisha akamnyamazia wa kumi. Watu wakasema: “Tunakuomba kwa ajili ya Allaah, ee Abul-A´war! Wewe ndiye wa kumi?” Akasema: “Mkiniomba kwa ajili ya Allaah, Abul-A´war ndiye wa kumi aliye Peponi.”
93 – Ahmad bin Harb ametukhabarisha: Qaasim ametukhabarisha: Israa’iyl ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Swilah bin Zufar, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, ambaye amesimulia:
”al-´Aqiyb na as-Sayyid wanaotokea Najraan walikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya kutaka walaaniane, ambapo mmoja wao akamwambia mwenziwe: ”Usimpe changamoto ya kulaaniana. Kwa sababu naapa kwa Allaah, kama kweli ni Mtume, basi pengine sisi na wale wataokuja baada yetu wasifaulu.” Wakasema: “Tumetimiza matakwa yako. Tutumie kwetu mtu mwaminifu kwelikweli.” Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakatazama juu, ambapo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Simama, ee Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah!” Alipoondoka akasema: ”Huyu ndiye mwaminifu wa ummah huu.”
94 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: Abu Daawuud al-Hafariy ametukhabarisha: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Swilah, kutoka kwa Hudhayfah, ambaye amesema:
”al-´Aqiyb na as-Sayyid wanaotokea Najraan walikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakasema: ”Tutumie kwetu mtu mwaminifu kwelikweli.” Watu wakapiga magoti, ambapo akasema: “Simama, ee Abu ´Ubaydah!”
95 – Naswr bin ´Aliy bin Naswr na Ismaa´iyl bin Mas´uud wametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid: Shu´bah ametuhadithia kwamba Abu Ishaaq amewakhabarisha: Nimemsikia Swilah bin Zufar akisema: Nimemsikia Hudhayfah akitaja:
”Watu wa Najraan walikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: ”Tutumie kwetu mtu mwaminifu kwelikweli.” Akasema: ”Nitawatumieni mtu mwaminifu kwelikweli. Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakatazama juu. Akamtuma Abu ´Ubaydah.”
96 – Ahmad bin Mas´adah ametukhabarisha, kutoka kwa Bishr bin al-Mufadhdhwal: Khaalid ametukhabarisha: Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ibn Abiy ´Adiy ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa Abu Qilaabah, ambaye amesema: Anas amesema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika kila ummah una mwaminifu wake, na hakika mwaminifu wa ummah huu ni Abu ´Ubaydah.”[1]
97 – ´Imraan bin Muusa ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Waarith: al-Jariyriy ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdullaah bin Shaqiyq, ambaye amesema:
”Nilimuuliza ´Aaishah: ”Ni Swahabah yupi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alikuw anapendeza zaidi kwake?” Akasema: ”Abu Bakr, kisha ´Umar na kisha Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah.” Nikasema: ”Kisha nani?” Akanyamaza.”[2]
98 – Muhammad bin Ismaa´iyl bin Ibraahiym na Muusa bin ´Abdir-Rahmaan (ambaye tamko ni lake) wametukhabarisha: Ja´far bin ´Awn ametukhabarisha, kutoka kwa Abu ´Umays, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah, ambaye amesimulia kuwa ´Aaishah aliulizwa:
”Ni nani ambaye Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angelimteua kuwa khaliyfah endapo angelifanya hivo?” Akasema: ”Abu Bakr.” Kisha akaambiwa: ”Ni nani baada ya Abu Bakr?” Akasema: ”´Umar.” Akaambiwa: ”Ni nani baada ya ´Umar?” Akasema: “Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah.” Kisha akaishilia hapo.”[3]
[1] al-Bukhaariy (3744) na Muslim (2419).
[2] at-Tirmidhiy (3657), ambaye amesema Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3657).
[3] Muslim (2385).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 76-79
- Imechapishwa: 13/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 76-79
Imechapishwa: 13/09/2026
https://firqatunnajia.com/21-fadhilah-za-abu-ubaydah-bin-al-jarraah/