Barua

بسم الله الرحمن الرحيم

السلام عليكم و رحمة الله و بركاته

Kupitia barua yenu nimeelewa kuwa yai la mwanamke kuliweka kwenye mirija ya kupimia ili kurutubishwa na mbegu za kiume. Kisha yai hilo hurudishwa kwenye fuko la uzazi la mwanamke ili mchakato wa utungisho uendelee. Jawabu langu ni kama ifuatavyo:

1 – Kitendo kitendo hakijuzu ikiwa hakihitajiki. Kwa sababu operesheni kama hiyo inapelekea kufunuliwa kwa uchi. Aidha, kuna khatari kwamba mirija ya uzazi itabadilika au kuvimba, ingawa ni kwa siku zijazo. Kwa kuongezea kwamba mtu kuyaacha mambo kwa asili yake kama yalivyo ni kufanya adabu kwa Allaah. Vilevile ndio bora na manufaa zaidi kuliko kutumia mbinu bunifu zilizovumbuliwa na viumbe ambazo pengine uzuri wake ukaonekana pale mwanzoni, lakini baadaye kukabaini kufeli kwake.

2 – Ikiwa kitendo hicho kinahitajika, basi naona kwamba kinafaa yatapotimia masharti matatu:

1 – Ni lazima upandikizaji wa mbegu uwe kwa manii ya mume na si mtu mwingine. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً

”Allaah amekufanyieni wake wanaotokamana na nyinyi wenyewe na amekufanyieni katika wake zenu watoto na wajukuu.”[1]

Watoto wanatakiwa kutokamana na waume tu.

2 – Utaratibu wa utoaji wa manii iwe kwa njia inayoruhusiwa kupitia kwa mwanamke wake, ima kwa njia ya kumpapasa au akamfanyisha punyeto.

3 – Ni lazima yai liwekwe ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke na haitofaa kuliweka kwenye tumbo la uzazi la mwanamke mwingine yeyote kwa hali yoyote ile. Kwani kufanya hivo kutapelekea kuingiza manii ya mwanamme ndani ya tumbo la mwanamke asiyekuwa halali kwake. Allaah (Ta´ala) amesema:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ

“Wake zenu ni konde kwenu. Hivyo ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo.”[2]

Mwanamke wa mtu pekee ndiye ambaye kafanywa kuwa shamba. Qur-aan, Sunnah na maafikiano katika hali hii vimefahamisha kuwa kijakazi anayo hukumu moja kama mke.

[1] 16:72

[2] 2:223

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/27-28)
  • Imechapishwa: 16/07/2026