Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kuhusu wale walioacha mfumo wao wamegawanyika makundi matatu: kundi la kwanza ni watu wanaofuata mawazo, la pili ni watu wanaopindisha maana na kundi la tatu ni watu wanaofuata ujinga. Kundi linalofata mawazo ni wanafalsafa pamoja na wale wanafalsafa na Suufiyyah wanaofuata njia yao.
MAELEZO
Watu wanaofuata mawazo ni wale wanaosema kuwa yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si hakika; bali ni mambo aliyoyawaza na kuwaonesha watu kwa ajili ya manufaa yao wenyewe.
Watu wanaopindisha maana ni wale wanaoyapa maandiko ya majina na sifa za Allaah tafsiri mbovu kutoka katika maana zake sahihi kwenda katika maana nyingine. Kama wanavyofanya Jahmiyyah, Mu´tazilah na waliokuja baada yao.
Wanaofuata ujinga ni wale Mufawwidhwah wanaosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui maana ya yale aliyoteremshiwa na Allaah katika majina na sifa. Wanasema hayo ni matamshi yasiyojulikana maana yake. Tunayayasoma na tunaiegemeza maana yake kwa Allaah. Kwa hiyo kwao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah hawakujua maana ya maandiko hayo – bali walitegemeza maana yake kwa Allaah.
Wanafalsafa ni wale wanaodai hekima na maarifa ya mambo. Lakini hawaamini Mitume. Bali wanaona kuwa wao wana elimu zaidi kuliko Mitume na kwamba wanajua yale ambayo Mitume hawakuyajua.
Mwanatheolojia (المتكلم) ni yule anayetoa hoja kwa kutumia elimu ya mabishano na falsafa katika mijadala na wala hatoi hoja kwa Qur-aan na Sunnah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 237
- Imechapishwa: 16/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kuhusu wale walioacha mfumo wao wamegawanyika makundi matatu: kundi la kwanza ni watu wanaofuata mawazo, la pili ni watu wanaopindisha maana na kundi la tatu ni watu wanaofuata ujinga. Kundi linalofata mawazo ni wanafalsafa pamoja na wale wanafalsafa na Suufiyyah wanaofuata njia yao.
MAELEZO
Watu wanaofuata mawazo ni wale wanaosema kuwa yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si hakika; bali ni mambo aliyoyawaza na kuwaonesha watu kwa ajili ya manufaa yao wenyewe.
Watu wanaopindisha maana ni wale wanaoyapa maandiko ya majina na sifa za Allaah tafsiri mbovu kutoka katika maana zake sahihi kwenda katika maana nyingine. Kama wanavyofanya Jahmiyyah, Mu´tazilah na waliokuja baada yao.
Wanaofuata ujinga ni wale Mufawwidhwah wanaosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui maana ya yale aliyoteremshiwa na Allaah katika majina na sifa. Wanasema hayo ni matamshi yasiyojulikana maana yake. Tunayayasoma na tunaiegemeza maana yake kwa Allaah. Kwa hiyo kwao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah hawakujua maana ya maandiko hayo – bali walitegemeza maana yake kwa Allaah.
Wanafalsafa ni wale wanaodai hekima na maarifa ya mambo. Lakini hawaamini Mitume. Bali wanaona kuwa wao wana elimu zaidi kuliko Mitume na kwamba wanajua yale ambayo Mitume hawakuyajua.
Mwanatheolojia (المتكلم) ni yule anayetoa hoja kwa kutumia elimu ya mabishano na falsafa katika mijadala na wala hatoi hoja kwa Qur-aan na Sunnah.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 237
Imechapishwa: 16/07/2026
https://firqatunnajia.com/144-wameacha-njia-ya-salaf/