Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Ni jambo linalotambulika kwa waumini ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mjuzi zaidi kuhusu hilo kuliko mwingine yeyote, kiumbe mwenye kuwatakia wengine mema zaidi na mwenye ufaswaha zaidi. Bali kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumekusanyika ukamilifu wa elimu, ukamilifu wa uwezo na ukamilifu wa matakwa. Ni jambo linalotambulika vyema kwamba pindi elimu, uwezo na utashi yanakamilika kwa yule mzungumzaji au mtendaji, basi maneno yake na matendo yake pia hukamilika. Hakika mambo yalivyo ni kwamba mapungufu hutokea ima kutokana na upugufu wa elimu yake au kwa kushindwa kwake kubainisha elimu yake au kwa kutotaka kubainisha. Sambamba na hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na upeo wa mwisho katika ukamilifu wa elimu, ukamilifu wa mwisho katika matakwa ya kubainisha na ukamilifu wa mwisho ya uwezo wa kubainisha kuliko wazi. Wakati uwezo huu kamili na matakwa yenye uamuzi yanapatikana kwa mtu, ndipo hufikiwa malengo. Kwa maana hiyo mtu akatambua kuwa malengo yake yalitimia pale alipozungumzia juu ya kumuamini Allaah na siku ya Mwisho, matakwa yake ni yenye kuafikiana na elimu yake na elimu yake juu ya ma mada hizo ilikuwa ndio elimu kamilifu zaidi. Kila mwenye kudhania kuwa kuna mwingine ambaye ni mjuzi zaidi wa mambo haya, ni mwenye kubainisha kwa ukamilifu zaidi au ni mwenye kupupia zaidi kuwaongoza watu kumshinda Mtume, basi mtu huyo ni katika makafiri na si katika waumini. Maswahabah, waliowafuata kwa wema na wale wenye kuwafuata Salaf wameongozwa katika jambo hili.
MAELEZO
Katika sifa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba yeye ndiye mwenye elimu zaidi miongoni mwa viumbe, mwenye ufaswaha zaidi kwa kuongea na mwenye kuwatakia kheri zaidi watu. Basi zikikusanyika kwake sifa hizi, basi ni lazima awabainishie watu. Kubainisha kwake mambo ya ´Aqiydah ni muhimu zaidi kuliko kubainisha hukumu za miamala na biashara, kwa sababu ´Aqiydah ndio msingi. Kwa hiyo hafichi chochote.
Kasoro huja aidha kwa uchache wa elimu, kwa kukosa uwezo wa kubainisha au kwa khiyana na kuficha. Haya yote hayapo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye mwenye elimu zaidi, mwenye ufaswaha zaidi na mwenye kuwatakia watu kheri zaidi. Mtu ambaye anawatakia watu kheri hafichi chochote kinachohitajika na ummah. Isitoshe anao uwezo wa kubainisha, kwa sababu yeye ndiye mwenye faswaha zaidi katika viumbe. Hakuna anayelingana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ufaswaha. Kumekusanyika kwake ukamilifu wa elimu na uwezo, navyo ni ufwasaha na ubainifu na pia utashi wa kubainisha na kutowaficha watu haki wala kuwafanyia ghushi. Ikiwa sifa hizi zitakamilika kwa asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi elimu yake, ubainifu wake na uwezo wake hukamilika. Basi vipi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye Allaah amemtuma, akambebesha ujumbe na kumuamrisha awabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwake? Inawezekanaje aache maudhui ya majina na sifa za Allaah bila kuubainisha mpaka waje hawa watu wawabainishie watu na kusema kuwa kilichokusudiwa ni hiki na kile na kudai kuwa haitakiwi kufahamika kwa maana yake ya dhahiri?
Haya ndiyo matokeo ya kukamilika sifa hizi kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nayo ni kukata kauli kuwa amewabainishia watu kila wanachokihitaji. Katika mambo ya mwanzo kabisa ni kuwa aliwabainishia watu majina na sifa za Allaah kwa namna isiyo na utata wala giza. Atakayemtuhumu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutobainisha na kwamba mwingine ana uwezo zaidi kuliko yeye katika kubainisha, khaswa inapokuja katika maudhui ya majina na sifa za Allaah, kama inavyopelekea ´Aqiydah ya Jahmiyyah na Mu´tazilah, basi huyo ni katika wazandiki na si katika waumini.
Maswahabah na wale waliopita katika njia yao miongoni mwa waliokuja baada yao katika mada ya majina na sifa za Allaah na mengineyo walikuwa juu ya uongofu. Kwa sababu wanaamini kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaletea haki, akaifikisha kwao na akaibainisha kwao. Hivyo wako juu ya njia iliyonyooka. Hali hiyo ni tofauti na wazandiki ambao wamemtuhumu Mtume kuwa hakubainisha yale yanayompasa na kumstahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 233-236
- Imechapishwa: 16/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 233-236
Imechapishwa: 16/07/2026
https://firqatunnajia.com/143-muhammad-mjuzi-mwenye-kuwatakia-watu-kheri-zaidi-na-mfaswaha/