Swali: Ni yepi maoni yako juu ya hirizi za Qur-aan zinazowekwa chini ya mito au zinaloweshwa na maji kisha baadaye zinanywewa?
Jibu: Ni jambo limesuniwa kutafuta matibabu kwa Qur-aan. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Kuna kikosi cha Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kilikuwa katika safari wakati walipotua kwenye kabila la mwarabu mmoja. Wakaomba wapokelewe kama wageni, lakini wakakataa. Mkuu wa kabila lile akawa amedungwa na nyoka. Wakajaribu kumtibu kwa kila njia, lakini haikusaidia kitu. Baadhi yao wakasema: “Nendeni kwa lile kundi lililokuja. Huenda wana kitu.” Wakaenda na kusema: “Mkuu wetu amedungwa na nyoka. Tumejaribu kumtibu kwa kila njia, lakini haikusaidia kitu. Je, kuna yeyote katika nyinyi ana chochote?” Mmoja wao akasema: “Ninaapa kwa Allaah ya kwamba nina tiba, lakini ninaapa kwa Allaah ya kwamba tumewaomba mtupokee kama wageni, lakini mmkakataa. Sintowatibu mpaka mtupe ujira kwa hilo.” Wakakubaliana kundi kadhaa la kondoo. Akaanza kumtemea cheche za mate na kusoma:
الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
“Himdi zote njema ni Zake Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]
Mtu yule akapata uchangamfu kana kwamba ameachwa huru kutokana na hatamu. Akaanza kutembea na kutohisi maumivu yoyote. Wakawapa ujira ambao walikubaliana. Baadhi yao wakasema: “Agawanywe.” Wengine wakasema: “Msifanye chochote mpaka tufike kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza yaliyopitika, tuangalie atatuamrisha nini.” Wakafika kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza yaliyopitika. Akasema: “Umejuaje kuwa [Suurah hii] inatibu?” Kisha akasema: “Mmefanya jambo la sawa. Mgaweni na mnipe sehemu” na akaanza kucheka.”[2]
Kuhusiana na hirizi ya Qur-aan, imejuzishwa na baadhi ya Salaf na wakaikataza wengine. Miongoni mwa ambao wameikataza ni pamoja na ´Abdullaah bin Mas´uud kama ambavo wako wanazuoni wengine walioijuzisha. Kuhusu kuweka hirizi ya Qur-aan chini ya mito au kuitundika kwenye ukuta ni mambo ambayo hayakupokelewa kutoka kwa Salaf. Hatutakiwi kufanya kitendo ambacho hakuna yeyote katika Salaf aliyetutangulia kukifanya. Baya zaidi kuliko hivyo ni yale yanayofanywa na baadhi ya watu ambapo wanayasomea maji yaliyo na zafarani na kisha wanaandika maandishi yasiyosomeka kwa maji hayo ya zafarani. Kitendo hicho ni Bid´ah na ni cha makosa.
[1] 01:01
[2] al-Bukhaariy (2276) na Muslim (2201).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/24-25)
- Imechapishwa: 16/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/24-25)
Imechapishwa: 16/07/2026
https://firqatunnajia.com/hirizi-ya-qur-aan-chini-ya-mito/