Swali: Je, kupaka wanja mchana wa Ramadhaan kunafunguza?

Jibu: Maoni yaliyo na nguvu ni kwamba wanja haumfunguzi. Haijalishi kitu hata kama atahisi rangi au ladha yake kwenye koromeo. Hayo yamehakikishwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Kwa sababu huku sio kula wala kunywa na wala hakuna maana ya kula na kunywa. Wala kitendo hichi hakifanani na yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Laqiytw bin Swabirah:

“Pitiliza katika kupalizia isipokuwa ikiwa umefunga.”

Kwa sababu pua ni mahali ambapo kunaweza kupitishwa vinywaji tumboni. Ni mahali kulikozoeleka kuingiza chakula. Ama jicho sivyo hivyo. Kwa ajili hii mfungaji ana ruhusa ya kupaka wanja japokuwa wanja utafika kwenye koromeo yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1564
  • Imechapishwa: 01/03/2020