Kuosha viungo vya wudhuu´ zaidi ya mara tatu

Swali: Je, inafaa kuosha viungo zaidi ya mara tatu katika kutawadha?

Jibu: Hapana, haitakikani. Dogo liwezalo kusemwa ni machukizo. Mara tatu pekee; uso mara tatu, mikono mara tatu na miguu mara tatu. Kuhusu kichwa apanguse mara moja. Hivo ndio Sunnah. Asizidishe mara tatu. Imekuja katika baadhi ya mapokezi:

”Atakayezidisha amefanya vibaya, amevuka mipaka na kufanya dhuluma.”

Sunnah wakati wa kutawadha ni mtu asizidishe mara tatu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24500/حكم-غسل-الاعضاء-اكثر-من-ثلاث-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 18/10/2024