Kuosha nguo kwa njia ya mvuke

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia nguo za najisi ambazo zimesafishwa kwa njia ya mvuke?

Jibu: Mvuke ni maji. Ikiwa mvuke una maji masafi na unaondosha athari ya najisi nguo zinakuwa safi. Ni lazima mvuke uwe na maji masafi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020