Kuongeza “wa Barakaatuh” katika salamu ya swalah

Swali: Kuongeza:

وبركاته

”… na baraka Zake.”

katika salamu baada ya kumaliza kuswali?

Jibu: Imepokelewa katika baadhi ya mapokezi ambayo baadhi yake yana udhaifu. Maoni yaliyo karibu zaidi na usahihi ni kuishilia:

رحمة الله

“… na rehema za Allaah.”

kama alivyosimulia Samurah ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

السلام عليكم ورحمة الله، السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu, Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

Swali: Nyongeza:

وبركاته

”… na baraka Zake.”

ni dhaifu?

Jibu: Ndio, inapingana na Hadiyth Swahiyh. Salamu ya kumaliza kuswali mtu aseme:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

Lakini mtu anaposalimiana na watu ndio kukamilifu zaidi. Nakusudia mtu anaposalimiana na watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23383/حكم-زيادة-وبركاته-في-السلام-من-الصلاة
  • Imechapishwa: 07/01/2024