Swali: Kuna muulizaji ametuma swali lake kwa kusema: “Nakuomba kwa jina la Allaah umsomee Shaykh swali langu.”

Jibu: Haitakikani kwa mtu kumtia uzito ndugu yake kwa kusema: “Nakuomba kwa jina la Allaah”. Hayo ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kukuombeni kwa jina la Allaah basi muitikieni.”

Ukimwambia mtu: “Nakuomba kwa jina la Allaah” umemtia uzito. Kwa sababu anabaki akiwa ni mwenye mashaka; akuitikie au asikuitikie. Huenda katika kukuitikia kwako kuna madhara kwake. Hivyo haitakikani kwa mtu kumuomba ndugu yake namna hii. Pamoja na kwamba wapo wanachuoni waliosema kwamba maana ya:

“Yule mwenye kukuombeni kwa jina la Allaah basi muitikieni.”

ni kwamba yule mwenye kukuombeni kwa dini ya Allaah au kwa msemo mwingine maombi ambayo yanafaa kwake, basi muitikieni. Kwa ajili hii nawanasihi ndugu zangu wote waislamu wasiwaambie nduguze: “Nakuomba kwa jina la Allaah”. Jengine ni kwamba huyu mwenye kuombwa ikiwa katika kuitikia kwake kuna madhara si lazima kuitikia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (72) http://binothaimeen.net/content/1658
  • Imechapishwa: 08/04/2020