Kuoga janaba siku ya ijumaa kabla ya alfajiri

Swali: Vipi ikiwa mtu ataoga janaba kabla ya adhaana ya Fajr na akanuia kuwa ni josho la siku ya ijumaa?

Jibu: Hapana, ikiwa ameoga kabla ya alfajiri, haisihi kama josho la ijumaa. Anatakiwa aoge siku ya ijumaa. Akioga kwa ajili ya janaba usiku kabla ya alfajiri, hiyo haitoshi. Inapendeza aoge josho la ijumaa baada ya adhaana anapokwenda msikitini kwa ajili ya ijumaa.

Swali: Vipi ikiwa ataoga baada ya alfajiri?

Jibu: Ikiwa ataoga baada ya alfajiri, inatosha. Akienda kuoga tena wakati wa kwenda kuswali ijumaa ni vizuri, kwa sababu kati ya Fajr na wakati wa kwenda ijumaa kuna muda.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31516/هل-يجزى-الغسل-قبل-الفجر-للجنابة-والجمعة
  • Imechapishwa: 25/10/2025