Kunyanyua mikono kwa ajili ya du´aa katika Twawaaf na Sa´y

Swali: Mtu anatakiwa kunyanyua mikono na kuomba du´aa hata kwenye mzunguko wa mwisho?

Jibu: Ndio, hata katika mzunguko wa mwisho katika Twawaaf na Sa´y. Sehemu zote mbili. Anatakiwa kunyanyua mikono yake na kuleta Takbiyr hata wakati wa mzunguko wa mwisho katika Twawaaf na vivyo hivyo wakati wa Sa´y kwenye Mawrah katika mzunguko wa mwisho atanyanyua mikono yake na kuomba du´aa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24995/حكم-رفع-اليدين-في-الدعاء-بالطواف-والسعي
  • Imechapishwa: 23/01/2025