Swali: Je, inajuzu kuomba du´aa kwa kuinua mikono baada ya swalah?
Jibu: Haina asili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiinua mikono baada ya kutoa salamu. Bali alikuwa akiomba du´aa baina yake na nafsi yake. Hivyo basi watu wasiinue mikono baada ya salamu, si baada ya Dhuhr, ´Aswr, Maghrib, ´Ishaa wala Fajr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakufanya hivyo. Ama mtu kuomba du´aa baina yake na nafsi yake baada ya Dhikr, hilo halina tatizo.
Swali: Vipi ikiwa ni baada ya swalah za Sunnah?
Jibu: Baada ya swalah za Sunnah, akifanya hivyo katika baadhi ya nyakati, hakuna tatizo. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiendelea kulifanya jambo hilo kila mara. Kwa hiyo akifanya mara moja na akaacha mara nyingine, ni vizuri, au ikamtokea du´aa fulani ambapo akaamua kuinua mikono na kuomba.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2451/حكم-رفع-اليدين-بالدعاء-عقب-الصلوات
- Imechapishwa: 29/03/2026
Swali: Je, inajuzu kuomba du´aa kwa kuinua mikono baada ya swalah?
Jibu: Haina asili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiinua mikono baada ya kutoa salamu. Bali alikuwa akiomba du´aa baina yake na nafsi yake. Hivyo basi watu wasiinue mikono baada ya salamu, si baada ya Dhuhr, ´Aswr, Maghrib, ´Ishaa wala Fajr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakufanya hivyo. Ama mtu kuomba du´aa baina yake na nafsi yake baada ya Dhikr, hilo halina tatizo.
Swali: Vipi ikiwa ni baada ya swalah za Sunnah?
Jibu: Baada ya swalah za Sunnah, akifanya hivyo katika baadhi ya nyakati, hakuna tatizo. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiendelea kulifanya jambo hilo kila mara. Kwa hiyo akifanya mara moja na akaacha mara nyingine, ni vizuri, au ikamtokea du´aa fulani ambapo akaamua kuinua mikono na kuomba.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2451/حكم-رفع-اليدين-بالدعاء-عقب-الصلوات
Imechapishwa: 29/03/2026
https://firqatunnajia.com/kunyanyua-mikono-kuomba-duaa-baada-ya-swalah-hakuna-msingi/