Kunyanyua kidole cha shahadah ndani ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu kwa mswaliji kunyanyua kidole cha shahadah wakati imamu anaposoma kwa sauti anapofika katika Aayah zinazozungumzia kumpwekesha na kumtukuza Allaah au mfano wa hayo? Je, akatazwe mwenye kufanya hivo ikiwa jambo hili halikuwekwa katika Shari´ah?

Jibu: Sijui msingi wa jambo hili. Kitendo katika ´ibaadah kinahitajia dalili. Kunyanyua kidole kunahitajia dalili na bora ni kuacha kufanya hivo. Mtu anatakiwa kuogopa kwa viungo vyake na kuvisikilizisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 20/10/2019