Kununua kwenye maduka yanayouza bidhaa za haramu

Swali: Kununua kutoka katika maduka yanayouza sigara na magazeti yanayoharibu kunazingatiwa ni katika kusaidiana katika dhambi na uadui?

Jibu: Kunachelewa hilo. Wale wanaouza sigara na magazeti haya wanatakiwa kunasihiwa. Wasipoitikia basi wanatakiwa kukatwa na wasinunue kutoka kwao. Wakisuswa na watu, watu wa kheri, wema na wanazuoni basi watalalamika na kuachana na mambo haya ya haramu. Lakini watu wakichukulia wepesi na wakawa ni wenye kununua kutoka kwao na wasijali, basi hilo litawapelekea kuzidi kufanya mambo hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 06/06/2021