03. ´Ibaadah kwa mwenye nifasi akisafika kabla ya arobaini

Swali 3: Ni lazima kwa wanawake wenye damu ya uzazi wafunge na kuswali wakisafika kabla ya siku arobaini?

Jibu: Ndio. Pindi mwanamke mwenye damu ya uzazi ataposafika kabla ya arobaini basi ni lazima kwake kufunga ikiwa hayo yamemtokea katika Ramadhaan. Aidha ni lazima kwake kuswali. Inafaa kwa mume wake kumjamii kwa sababu ni msafi. Hana kitu kinachomzuia kufunga, ulazima wa swalah na uhalali wa jimaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 8-9
  • Imechapishwa: 06/06/2021