Kununua katama kwa ajili ya Uddhiyah

Swali: Nataka kununua katama kuanzia sasa na kumlea. Akigonjweka, akavunjika au akapatwa na kitu ambacho ni kikwazo katika Udhhiyah nimchinje au nisimchinje pamoja na kuzingatia ya kwamba namnunua kuanza sasa?

Jibu: Wanachuoni (Rahimahu Allaah) amesema “iwapo utamuanisha na kusema kwamba huyu ni wa Udhhiyah anakuwa Udhhiyah. Akipatwa na maradhi au akavunjika ikiwa wewe ndiye msababishaji basi hasihi. Katika hali hii itawajibika ununue badala yake mfano wake au ambaye ni mbora kuliko huyo. Ikiwa wewe si msababishaji basi anasihi.”

Kutokana na hili tunasema bora zaidi ni mtu asubiri katika kule kuanisha. Kwa mfano anaweza kumnunua mapema kwa ajili ya kumpa chakula kilicho kizuri zaidi, lakini asimuanishe. Pale itapofika wakati wa kuchinja ndio amuanishe na kusema:

اللهم هذا منك ولك عني وعن أهل بيتي

“Ee Allaah! Huyu ni kutoka Kwako na ni Wako kwa ajili yangu mimi na watu wa nyumba yangu.”

Asipomuanisha anafaidi faida muhimu; akitaka kumwacha na kununua mwingine inafaa kwake kufanya hivo kwa sababu hakumuanisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/976
  • Imechapishwa: 16/12/2018