Swali: Kuna mtu amenuia kufunga kila jumatatu na alkhamisi lakini hakuweka nadhiri ya jambo hilo. Je, analazimika kuyafunga masiku hayo maisha yake yote?

Jibu: Kuweka nia ya kitendo peke yake hakulazimishi kitendo. Mtu akinuia kufunga jumatatu na alkhamisi na baadaye akaacha kufanya hivo, hakuna kinachomlazimu. Vivyo hivyo akianza kufunga kisha baadaye akaikata swawm yake hakuna kinachomlazimu, kwa sababu funga inayopendeza hailazimu kuikamilisha. Hata kama mtu atanuia kutoa swadaqah ya pesa na akatenga kiwango hicho pembeni; haimlazimu kuitoa swadaqah. Nia haina athari yoyote katika mambo kama haya. Kutokana na haya tunamwambia ndugu muulizaji kwamba haimlazimu kuiendelea kufunga jumatatu na alkhamisi. Lakini akifanya hivo ni vyema kwa sababu imesuniwa kufunga jumatatu na alkhamisi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/16-17)
  • Imechapishwa: 30/03/2026