Swali: Nikiingia msikitini na kukuta imamu yuko katika mwisho wa swalah, karibu kutoa salamu, na niko pamoja na wenzangu – Je, tujiunge nyuma ya imamu au tuswali mkusanyiko peke yetu? Ni ipi dalili inayoonyesha kuwa Takbiyrat-ul-Ihraam inatosha badala ya Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´ mtu akijiunga na imamu akiwa tayari yuko katika Rukuu´?
Jibu: Hili alilouliza swali lina upana wa hukumu kwa idhini – Allaah akitaka. Lakini dhahiri ya Hadiyth inaonyesha kuwa mtu anapaswa kujiunga pamoja na imamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile mlichowahi, kiswalini, na kile mlichokosa, kikamilisheni.”
Imekuja katika riwaya nyingine:
“Kilipeni.”
Hivyo yule mwenye kujiunga kabla imamu hajatoa slaamu, basi amepata sehemu ya swalah na hivyo na anaingia katika maana ya maneno yake:
“Kile mlichowahi, kiswalini.”
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mnaposikia Iqaamah basi tembeeni kwa utulivu na kwa staha. Kile mlichowahi, kiswalini, na kile mlichokosa, kikamilisheni.”
Hii inawahusu wote wanaoingia katika Rak´ah ya kwanza, ya pili, ya tatu au ya nne, au hata wakati wa Tashahhud. Kwa hiyo wakiingia na imamu na wakakaa katika Tashahhud na wakafanya sujuud ya mwisho pamoja naye, basi hilo ndilo bora zaidi na linaafikiana na dhahiri ya Sunnah.
Hata hivyo wakiamua kuswali mkusanyiko wao baada ya salamu ya imamu katika sehemu yoyote ndani ya msikiti, inatarajiwa hakuna tatizo. Lakini ushauri wangu na ninachokiona kuwa ndicho salama zaidi na Sunnah ni kwamba wajiunge na imamu hata kama swalah iko mwishoni, kwa mujibu wa Hadiyth:

Ama maneno ya baadhi ya wanazuoni kwamba Takbiyrat-ul-Ihraam inatosha badala ya Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´, msingi wake ni kwamba ´ibaadah hizi mbili ni katika aina moja na hivyo ´ibaadah ndogo inaingia katika ´ibaadah kubwa. Kwa maana mtu akisema “Allaahu Akbar” kwa ajili ya kuingia katika swalah na akakuta imamu yuko katika Rukuu´, basi Takbiyr hii moja inahesabiwa kuwa imekidhi pia Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´. Hii ni kwa sababu hizi ni ´ibaadah mbili zilizokutana kwa wakati mmoja na mtu anakhofia kutamka ya pili anaweza kuikosa Rak´ah. Mfano wa jambo hili ni mtu anapoingia msikitini na akawa anataka kuswali Rak´ah mbili za Sunnah ya Raatibah. Rak´ah hizo zinamtosheleza pia kwa swalah ya mamkizi ya msikiti. Vivyo hivyo mtu akiingia msikitini na watu wanaswali swalah ya faradhi, anaingia moja kwa moja katika swalah ya faradhi, nayo inamtosheleza kwa swalah ya mamkizi ya msikiti.
Kadhalika mtu akioga josho la janaba kwa nia ya kuondoa janaba na wudhuu´ kwa pamoja, basi josho hilo linamtosheleza, kwani wudhuu´ ni ´ibaadah ndogo ambayo inaingia katika ´ibaadah kubwa. Kwa msingi huo baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walitoa fatwa kuwa Takbiyrat-ul-Ihraam inatosha badala ya Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´ ili mtu asipoteze Rak´ah. Hii ni kwa kulipa umuhimu lililo kubwa na kuacha dogo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1114/حكم-من-اتى-جماعة-والامام-في-التشهد-الاخير
- Imechapishwa: 17/08/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1114/حكم-من-اتى-جماعة-والامام-في-التشهد-الاخير
Imechapishwa: 17/08/2026
https://firqatunnajia.com/kundi-la-watu-wamemkuta-imamu-katika-tashahhud-ya-mwisho/