Allaah (Ta´ala) amesema:
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ
“Ndivyo hivyo na yeyote anayeadhimisha ´ibaadah za Allaah, basi hayo ni katika uchaji wa nyoyo.”[1]
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ
“Ndio hivyo iwe na yeyote anayetukuza vitukufu vya Allaah, basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Mola wake.”[2]
وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ
”… na inamisha bawa lako kwa waumini… ”[3]
وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا
“Wale wanaowaudhi waumini wa kiume na waumini wa kike pasi na wao kufanya kosa lolote, basi kwa hakika wamejibebea uzushi mkuu wa dhuluma na dhambi ya wazi.”[4]
Katika mlango huu ipo Hadiyth ya Abu Mas‘uud al-Answaariy na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas zilizotangulia.
Abu Muusa al-Ash‘ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika katika kumtukuza Allaah (Ta´ala) ni kumheshimu mzee muislamu mwenye mvi, mbebaji wa Qur-aan ambaye hapindukii mipaka ndani yake wala hazembei, na kumheshimu kiongozi mwadilifu.”[5]
Ameipokea Abu Daawuud na Hadiyth ni nzuri.
‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha tuwape watu daraja zao.”[6]
Ameipokea Abu Daawuud katika ”as-Sunan” yake, na al-Bazzaar katika ”al-Musnad”. al-Haakim Abu ´Abdillaah amesema katika ”‘Uluum-ul-Hadiyth” ya kwamba Hadiyth ni Swahiyh. Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwakusanya watu wawili katika waliouawa katika vita vya Uhud, kisha akasema: ”Ni yupi kati yao alikuwa anayejua Qur-aan zaidi?” Basi akiashiriwa mmoja wao, humtanguliza kwenye mwanandani.”[7]
Ameipokea al-Bukhaariy.
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah (‘Azza wa Jall) amesema: ”Yeyote atakayemdhuru walii wangu, basi Nimemtangazia vita.”[8]
Ameipokea al-Bukhaariy.
Aidha imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
”Yeyote atakayeswali Subh yuko katika ulinzi wa Allaah (Ta´ala). Hivyo basi asije Allaah akakudai kwa chochote katika ulinzi Wake.”[9]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Maimamu wawili wakubwa Abu Haniyfah na ash-Shaafi‘iy (Rahimahumaa Allaah) wamesema:
”Ikiwa wanazuoni si mawalii wa Allaah, basi Allaah hana walii kabisa.”
Haafidhw Abul-Qaasim bin ‘Asaakir (Rahimahu Allaah) amesema:
”Tambua, ee ndugu yangu – Allaah Atupe sisi na wewe tawfiyq ya kufikia radhi Zake na atujaalie kuwa miongoni mwa wanaomkhofu na kumcha ipasavyo – ya kwamba nyama za wanazuoni zina sumu na desturi ya Allaah katika kufichua aibu za wanaowapunguza hadhi zao inajulikana, na kwamba yeyote anayefungua ulimi wake dhidi ya wanazuoni kwa kuwatukana, basi Allaah humuadhibu kabla ya kufa kwake kwa kufa kwa moyo. Kwa hiyo waogope wale wanaokwenda kinyume na amri yake wasije wakapatwa na fitina au wakapatwa na adhabu chungu.”[10]
[1] 22:32
[2] 22:32
[3] 15:88
[4] 33:58
[5] Abu Daawuud (4843) na al-Bukhaariy katika “al-Adab al-Mufrad” (357). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4843).
[6] Abu Daawuud (4842). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (4842).
[7] al-Bukhaariy (1343, 1345, 1346, 1347, 1348, 1353 na 4079), Abu Daawuud (3138), at-Tirmidhiy (1036), an-Nasaa’iy (1955) na Ibn Maajah (1513).
[8] al-Bukhaariy (6502).
[9] Muslim (657).
[10] Tanbiyhu Kadhib-il-Muftariy, uk. 18.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 22-23
- Imechapishwa: 17/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 22-23
Imechapishwa: 17/08/2026
https://firqatunnajia.com/06-msomaji-wa-qur-aan-anapaswa-kuheshimiwa-na-kutoudhiwa/