Imethibiti kutoka kwa Abu Mas‘uud al-Answaariy al-Badriy (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Awaongoze watu katika swalah yule anayesoma vizuri zaidi Kitabu cha Allaah.”[1]
Ameipokea Muslim.
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
”Wasomaji wa Qur-aan na washauri ndio waliokuwa watu wa baraza la ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anh), ni mamoja iwe ni wazee au vijana.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake. Zitakuja katika mlango unaofuata baada ya huu Hadiyth zinazoingia katika mlango huu.
Tambua ya kwamba maoni sahihi na yaliyochaguliwa, ambayo wanayategemea wanazuoni ni kwamba kusoma Qur-aan ndio bora zaidi kuliko Tasbiyh, Tahliyl na aina nyingine za Adhkaar, jambo ambalo linafahamishwa na dalili – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
[1] Muslim (673).
[2] al-Bukhaariy (4642) na (7286).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 21
- Imechapishwa: 17/08/2026
Imethibiti kutoka kwa Abu Mas‘uud al-Answaariy al-Badriy (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Awaongoze watu katika swalah yule anayesoma vizuri zaidi Kitabu cha Allaah.”[1]
Ameipokea Muslim.
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
”Wasomaji wa Qur-aan na washauri ndio waliokuwa watu wa baraza la ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anh), ni mamoja iwe ni wazee au vijana.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake. Zitakuja katika mlango unaofuata baada ya huu Hadiyth zinazoingia katika mlango huu.
Tambua ya kwamba maoni sahihi na yaliyochaguliwa, ambayo wanayategemea wanazuoni ni kwamba kusoma Qur-aan ndio bora zaidi kuliko Tasbiyh, Tahliyl na aina nyingine za Adhkaar, jambo ambalo linafahamishwa na dalili – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
[1] Muslim (673).
[2] al-Bukhaariy (4642) na (7286).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 21
Imechapishwa: 17/08/2026
https://firqatunnajia.com/05-msomaji-zaidi-wa-qur-aan-ndio-mwenye-kupewa-kipaumbele/