Tumesimuliwa pia kupitia kwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) kwa tamko lisemalo:
”Hakuna husuda isipokuwa katika mambo mawili: mtu ambaye Allaah amempa mali, kisha akamuwezesha kuitumia katika haki, na mtu mwingine ambaye Allaah amempa hekima, basi anahukumu nayo na anaiwafundisha watu.”
´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yule mwenye kusoma herufi moja ndani ya Kitabu cha Allaah, basi analo jema moja – na jema moja linazidishiwa mara kumi. Sisemi kwamba Alif Laam Miym ni herufi moja, bali Alif ni herufi, Laam ni herufi na Miym ni herufi.”[1]
Ameipokea Abu ´Iysaa Muhammad bin ´Iysaa at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri, Swahiyh na ngeni kupitia njia hiyo.
Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mola (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema: ”Yule ambaye Qur-aan na kunitaja Kwangu kutamshughulisha kutokana na kuniomba, basi Nitampa bora kuliko ninavyowapa wenye kuomba. Ubora wa maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) juu ya maneno mengine yote ni kama ubora wa Allaah (Ta´ala) juu ya viumbe Vyake.”[2]
Ameipokea at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni.
Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika yule ambaye ndani ya kifua chake hakuna chochote katika Qur-aan ni kama nyumba iliyoharibika.”[3]
Ameipokea at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ataambiwa mtu wa Qur-aan: ”Soma, panda daraja na soma kwa utaratibu kama ulivyokuwa unasoma duniani. Kwani daraja lako litakuwa kwenye Aayah ya mwisho utakayoisoma.”[4]
Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa ni nzuri na Swahiyh, na an-Nasaa´iy.
Mu´aadh bin Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mwenye kuisoma Qur-aan na akaifanyia kazi kimatendo kwa yaliyomo ndani yake, basi Allaah atawavisha wazazi wake taji siku ya Qiyaamah. Mwanga wake ni bora kuliko mwanga wa jua katika nyumba za dunia. Basi mnaonaje kuhusu yule anayefanyia kazi hayo?”[5]
Ameipokea Abu Daawuud.
ad-Daarimiy amepokea kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:
”Someni Qur-aan, kwani Allaah (Ta´ala) hatauadhibu moyo uliobeba Qur-aan. Hakika hii Qur-aan ni karamu ya Allaah. Yule mwenye kuingia ndani yake yuko salama, na mwenye kuipenda Qur-aan basi na apewe bishara njema.”
´Abdul-Hamiyd al-Hammaaniy amesema:
”Nilimuuliza Sufyaan ath-Thawriy kuhusu mtu anayekwenda kupigana jihaad au ambaye anasoma Qur-aan, ni lipi linalokupendeza zaidi?” Akasema: ”Kusoma Qur-aan, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mbora wenu ni yule anayejifunza Qur-aan na akaifundisha.”
[1] at-Tirmidhiy (2910). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2910).
[2] at-Tirmidhiy (2926). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2926).
[3] at-Tirmidhiy (2913) na Ibn Maajah (217). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2913).
[4] at-Tirmidhiy (2914) na Abu Daawuud (1464). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2914).
[5] Abu Daawuud (1453). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1453).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 18-20
- Imechapishwa: 17/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 18-20
Imechapishwa: 17/08/2026
https://firqatunnajia.com/04-malipo-juu-ya-kila-herufi-inayosomwa-ya-qur-aan/